Tuesday, July 9, 2013

MAGAZETI LEO YA UDAKU via GLOBAL PUBLISH

Habari za wema Sepetu
MWIGIZAJI wa Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amewapongeza waandaaji wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 kwani lilikuwa zuri kuliko matamasha mengine yaliyowahi kutokea Bongo.

Akizungumza na paparazi wetu, Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Taifa lilipofanyika tamasha hilo, Dude alimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo kwa ubunifu wake kwani tamasha hilo limefanikiwa kuwaweka watu pamoja na kuwafanya wasahau tofauti zao za kidini, kivyama na kikabila.

“Kwa kweli tamasha hili ni zuri sana kwani limetusogeza karibu na tumesahau tofauti zetu na tupo pamoja, tunazungumza na kufurahia, nawapongeza sana Global Publishers na Shigongo kwa ubunifu kwani tamasha liko tofauti na mengine, Mungu ibariki Tanzania,” alisema…

POLISI WAVAMIA NYUMBANI KWA WEMA

Na Mwaija Salum

POLISI wapatao sita Jumamosi iliyopita walivamia nyumbani kwa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu maeneo ya Kijitonyama kwa lengo la kumkamata kufuatia kesi iliyofunguliwa katika Kituo cha Polisi Kawe jijini Dar.

Awali taarifa zilidai kuwa, tuhuma zinazomkabili staa huyo asiyekaukiwa na matukio ni za kumtukana na kumpiga vibao Godluck Kuyumbu ambaye ni meneja wa hoteli moja maarufu jijini Dar.

Baada ya kesi hiyo yenye jalada KW/RB5988/2013 SHAMBULIO kufunguliwa kituoni hapo Julai 6, mwaka huu mishale ya saa 5 asubuhi, maafande hao wakiwemo wa kike wawili wakiwa wamevaa kiraia walifika mtaa anaoishi staa huyo na kuufunga kabla ya kwenda kugonga katika geti la nyumba yake.

Mara baada ya kugonga geti hilo, alitoka mwanaume aliyefahamika kwa jina la Petman,…

SUMAYE ANOGESHA SEND-OFF YA NATASHA

Pos
Imelda Mtema na Hamida Hassan

WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Fredrick Sumaye, mwishoni wa wiki iliyopita aliinogesha sherehe ya kuagwa ‘Send Off’ ya  mwigizaji wa kitambo na

Mtangazaji wa Radio Times, Suzan Lewis ‘Natasha’.

Waziri mkuu huyo aliambatana na viongozi wengine wa kitaifa akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Hemed Kipozi, katika  Uwanja wa Mnazi Mmoja ilipofanyika sherehe hiyo iliyopewa jina la ‘Natasha Night’.

Sumaye pamoja na viongozi wengine hawakuwa nyuma katika kulisakata rumba pale zilipopigwa nyimbo za zamani ‘zilipendwa’. ‘MC’ aliwataka wageni waalikwa kujumuika pamoja na kupanda jukwaani kwa ajili ya kuserebuka, nao hawakujivunga.

Mbali na Sumaye na Kipozi, mastaa mbalimbali wa filamu wa hapa nchini walijitokeza kumpa kampani…

LOWASSA AZUA GUMZO

Na Mwandishi Wetu

ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya kuanza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, picha za Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM, Edward Lowassa akiwa amevaa mavazi ya Kiislam ya joho na hagali zimezua gumzo kubwa kwenye jamii wengi wakitaka kujua kama Waziri Mkuu Mstaafu huyo amebadili imani au la!

GUMZO LENYEWE

Picha hizo za Lowassa ambazo zimeenea mtandaoni, zimepokea maoni mbalimbali huku wengi wakiwa na maswali yaliyokosa majibu ya moja kwa moja.

Hata hivyo, asili ya picha hizo zilizombadilisha mwonekano Lowassa ni mtandao mmoja wa kijamii ambao umetupia picha na maelezo kwamba, mbunge huyo ambaye kasi yake ya kisiasa nchini haishikiki, alikuwa akipongezwa na Kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawi kwa kumvika joho na…

MAFUTA YA UBUYU WENGI KUFA GHAFLA


Ubuyu.
Na Mwandishi Wetu

SIKU chache baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kutangaza kwamba mafuta ya ubuyu hayafai kwa matumizi ya binaadamu,  taarifa hiyo imewafanya watu wengi kukumbwa na  hofu ya vifo vya ghafla.

Mafuta ya ubuyu.
Hofu hiyo inatokana na kuamini kwa muda mrefu kwamba mafuta hayo yamekuwa ni tiba asilia na salama kwa magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana mahospitalini.

No comments:

Post a Comment